Sera hii inaeleza jinsi Optiza Academy, sehemu ya Optiza Digital iliyopo Dar es Salaam, inavyokusanya, kutumia na kulinda taarifa zako unapotembelea academy.optiza.co.tz au unaponunua kozi, ebook au training kutoka kwetu.
1. Taarifa tunazokusanya
- Unapowasiliana nasi kwenye WhatsApp: jina lako, namba ya simu na ujumbe unaotutumia.
- Unapolipia: jina la muamala au uthibitisho wa malipo unaotutumia. Hatuombi wala kupokea PIN, nywila au taarifa za akaunti yako ya benki au simu.
- Ili kukupa kozi au ebook: barua pepe au namba ya simu unayotumia kwenye Selar, ili tukuongeze kwenye kozi au tukutumie kitabu.
- Taarifa za kiufundi: anwani ya IP, aina ya kifaa na kivinjari, ambazo seva ya tovuti hukusanya kwa ajili ya usalama na kuzuia mashambulizi.
2. Jinsi tunavyotumia taarifa zako
- Kuthibitisha malipo yako na kukupa kozi, ebook au training uliyonunua.
- Kujibu maswali yako na kukupa msaada.
- Kukujulisha kozi au bidhaa mpya, pale tu ulipoomba (kwa mfano kwa kubonyeza “Nijulishe ikitoka”).
- Kulinda usalama wa tovuti na wateja wetu.
3. Huduma za watu wengine
Tunatumia huduma za makampuni mengine ili kukuhudumia, na kila moja lina sera yake ya faragha:
- WhatsApp (Meta): mawasiliano na wateja.
- Selar: kutoa kozi na ebooks.
- M-Pesa na NMB: kupokea malipo.
- YouTube: video za ushuhuda kwenye tovuti. YouTube inaweza kuweka cookies unapocheza video.
4. Cookies
Tovuti hii yenyewe haitumii cookies za matangazo. Cookies chache zinaweza kuwekwa kwa ajili ya usalama wa tovuti, au na YouTube unapocheza video. Unaweza kuzuia au kufuta cookies kupitia mipangilio ya kivinjari chako.
5. Hatuuzi taarifa zako
Hatuuzi, hatukodishi wala hatugawi taarifa zako kwa mtu yeyote kwa ajili ya matangazo yao. Tunazishiriki tu na huduma zilizotajwa hapo juu, kwa kiwango kinachohitajika kukuhudumia, au pale sheria inapotutaka kufanya hivyo.
6. Muda wa kuhifadhi taarifa
Tunahifadhi taarifa zako kwa muda unaohitajika kukupa huduma, na kwa muda unaotakiwa kisheria kwa kumbukumbu za kibiashara na kodi. Baada ya hapo tunazifuta.
7. Haki zako
Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania, una haki ya:
- Kuomba kuona taarifa zako tulizonazo.
- Kuomba tusahihishe taarifa zisizo sahihi.
- Kuomba tufute taarifa zako, pale ambapo hatulazimiki kisheria kuzihifadhi.
- Kuacha kupokea ujumbe wa matangazo kutoka kwetu wakati wowote.
Kutumia haki hizi, wasiliana nasi kupitia WhatsApp hapa chini.
8. Mabadiliko ya sera hii
Tunaweza kubadilisha sera hii mara kwa mara. Tarehe iliyo juu ya ukurasa huu inaonyesha ilipobadilishwa mara ya mwisho.
9. Wasiliana nasi
Optiza Digital, Dar es Salaam, Tanzania
WhatsApp: +255 658 145 285